Kiongozi wa chama hicho Bouguerra Sultani amesema kuwa chama chake kinataka mfumo wa Bunge ambapo Bunge la wananchi litakuwa na uwezo wa kutoa maamuzi muhimu na wala sio mfumo wa utawala ambapo Rais ndiye mwenye mamlaka kamili. Sultani amesema uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo utatolewa mwishoni mwa mwezi huu baada ya baraza kuu kuketi na kushauriana.Kuondoka chama hicho serikalini hakutasambaratisha serikali ya Algiers lakini weledi wa siasa za nchi hiyo wanaitakidi kuwa hatua kama hiyo itakuwa pigo kubwa kwa Rais Abdul Aziz Bouteflika na serikali yake.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 286606
Chama cha Kiislamu nchini Algeria kimesema kinajiandaa kuondoka serikalini ili kupigania mageuzi ya kimsingi ikiwemo kupunguzwa mamlaka ya Rais.